Animal husbandry: Ufugaji

UTANGULIZI

Ufugaji ni shuguli za utunzaji wa mifugo mbali mbali wa majumbani kwetu kwa ajili ya uzalishaji chakula (kwa mazao yao mf. maziwa, nyama, mayai), nguvu kazi, ulinzi au biashara.  Wanyama au ndege tunaowafuga wanaitwa kwa ujumla mifugo. mfano wa mifugo hapa nchini ni kama vile ng'ombe, mbuzi, kondoo, puda, farasi, sungur, simbirisi nakadhalika pia kuna ndege wafugwao kama vile kuku, bata, batamzinga, kanga, njiwa n.k. Kuna wanyama kama mbwa na paka ambao hufugwa kama walinzi au urembo. Pia kuna wanyama au ndege wa porini ambao hufugwa pia na binadamu kwa lengo la kibiashara au urembo mfano ndege kasuku, tausi na wanyama kama vile kobe, nyoka n.k.